Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vybz Kartel aliyefungwa jela maisha, ana hali mbaya

Kartel Vybz Kartel

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki toka nchini Jamaica Vybz Kartel anapambana na ugonjwa ambao unatishia uhai wake wakati akitumikia kifungo cha maisha Jela. Kwa mujibu wa FOX 5 New York, Kartel anasumbuliwa na (Graves’ Disease) maradhi ya kutisha kwenye Koo pamoja na hali ya moyo wake haipo sawa.

Nyaraka za hospitali zilizonaswa na mtandao huo zinadai, afya yake inazidi kuzorota na huwenda ikawa mbaya zaidi kama hatopewa matibabu ya haraka ikiwemo kufanyiwa upasuaji. Daktari wake binafsi ndiye ametoa taarifa kwa mamlaka husika juu ya hali ya Kartel.

Mkali huyo wa Dancehall anatumikia kifungo cha maisha katika gereza la nchini Jamaica kufuatia kukutwa na hatia ya mauaji mwaka 2014.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live