Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vybz Kartel aliachiliwa baada ya hukumu ya mauaji kubatilishwa

Vybz Kartel Aliachiliwa Baada Ya Hukumu Ya Mauaji Kubatilishwa.png Vybz Kartel aliachiliwa baada ya hukumu ya mauaji kubatilishwa

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Msanii wa dancehall kutoka Jamaica, Vybz Kartel ameachiliwa huru kutoka gerezani baada ya majaji kuamua kwamba hapaswi kushtakiwa tena kwa mauaji.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 48, ambaye jina lake halisi ni Adidja Palmer, alifungwa mwaka 2014 lakini hukumu yake imebatilishwa na majaji wa Uingereza mwezi Machi.

Alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji ya Clive "Lizard" Williams nchini Jamaica lakini amekuwa akisisitiza kuwa hana hatia.

Ingawa hukumu yake libatilishwa miezi kadhaa iliyopita na jopo la mahakama ya Privy mjini London, mamlaka nchini Jamaica ilikuwa na muda wa kuamua kama angeshtakiw tena au la.

Siku ya Jumatano, majaji wa mahakama ya rufaa nchini Jamaica waliamua kesi hiyo isirudishwe mahakamani, ikimaanisha kwamba Kartel, ambaye anasemekana kuwa na afya mbaya, anaweza kuachiliwa.

Chanzo: Bbc