Mfanyabiashara Fred Ngajiro 'Vunja Bei' ametaja sababu ya kuzungumzia ishu ya Tunda na Whozu katika masuala yao ya mahusiano.
Fred amefunguka hayo mara baada ya kuulizwa kuwa, haoni kama kuna tatizo kuzungumzia penzi hilo jambo ambalo limemfanya Tunda aibuka na kumjibu kwenye mitandao ya kijamii.
"Sijaona alichojibu Tunda sababu nilikuwa bize na uzinduzi wa duka langu hili la Kigoma, nitaingia baadaye nitaona. Lakini kwa nini namzungumzia Whozu, huyu ni kijana wangu, ni msanii wangu yupo Too Much Money.
"Na nilisema, mimi nianachofahamu ni kwamba kila mtu alishindwa kuendelea na mwenzake sasa hayo ya sijui nani alimuacha mwenzake mimi iswezi kuyajua sababu mimi sio mtu wao wa tatu wa mahusiano," alisema Vunja.