Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Voice Wonder kurejea na kishindo kikubwa

Voice Wonder Voice Wonder.

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Nimpende Nani’, Voice Wonder amedai kuwa hahofii kurudisha tena nafasi yake kimuziki kwakuwa licha ya muziki kubadilika mchezo anaujua vyema.

Pia, anadai alichojifunza kwenye muziki wa sasa ni kuwa idea za nyimbo nyingi zinafanana kuanzia mashairi na melody hivyo hakuna kinachomshtua.

“Mimi nimefanya muziki kipindi kuna watu wazito na nikapenya, akina Juma Nature, Inspekta wa moto, Chilla, Bushoke wa mtoto, Banana, K Bazil na bado unafanya kitu watu wanajua huyu ni Voice, huyu ni Banana, huyu ni Bushoke kunakuwa na tofauti.

"Mtu anasikia anajua huyu ni fulani na bado soko halikuwepo gumu kwa upande wangu. Sioni kama kuna wasanii wawili watatu wanasumbua mimi nikashindwa kupenya pale kati,” amesema Voice Wonder.

Amesisitiza kuwa muziki wake sasa hivi una mabadiliko makubwa kwakuwa amekuwa kimuziki na kiumri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live