Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vitu vinapikwa: Zuchu atua Afrika Kusini kuungana na bosi wake Diamond Platnumz

29e68ceec1cc7a69 Vitu vinapikwa: Zuchu atua Afrika Kusini kuungana na bosi wake Diamond Platnumz

Mon, 10 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Zuchu alisafiri kwenda Afrika Kusini kuungana na bosi wake Diamond Platnumz

- Totoshoo huyo ni miongoni mwa wasanii waliosainiwa na lebo ya Wasafi Records inayomilikiwa na Diamond Platnumz

- Diamond Platnumz anaandaa albamu ambayo inaonekana huenda ikamjumuisha Zuchu na wasanii wengi aliowasaini

- Sio Zuchu peke yake ambaye ameingia Afrika Kusini. Rayvanny pia alikuwepo siku chache zilizopita

Kiongozi wa kundi la lebo ya Wasafi Records Diamond Platnumz huenda atakaa kwa muda mrefu Afrika Kuisini akifanya kazi.

Kulingana na ratiba ya shughuli zake, mwanamuziki huyo anaonekana kuwa na mipango ya kukaa nje ya Tanzania kwa muda na alikuwa amejiandaa vilivyo, na hii imethibitishwa kutokana na wasanii chini yeke kusafiri na kuungana naye mmoja baada ya mwingine.

Katika wasanii hao ni totoshoo Zuchu ambaye kwa sasa hivi yupo Afrika Kusini baada ya kutua usiku wa Jumamosi, Mei 8.

Diamond Platnumz anaandaa albamu ambayo inaonekana huenda ikamjumuisha Zuchu na wasanii wengi aliowasaini. Hii inatarajiwa kuwa albamu ya hadhi kubwa na tayari mashabiki wake wanamsubiri kwa hamu ili amalize na kuiachia hewani.

Sio Zuchu peke yake ambaye ameingia Afrika Kusini. Rayvanny pia alikuwepo siku chache zilizopita.

Rayvanny ambaye jina lake halisi ni Raymond Shaban Mwakyusa, alikuwa na mipango mingi. Alifichua kuwa, atakuwa kwenye albamu ya Diamond Platnumz na pia alikuwa akishoot video ya muziki nchini Afrika Kusini.

Siku chache baadaye, meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale pia alienda kumtembelea Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Wasafi.

Kwa sasa zamu ni yake Zuchu kukanyaga katika mitaa ya Afrika Kusini. Chochote anachopanga kufanya nchini humo kando na muziki, tutasubiri tu kikiona ama kukisikia.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke