Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita yasababisha Tamasha la Bruno Mars kufutwa

Bruno Mars 100823 6 351d0469da294a0f8f6e15e4f872e030 Vita yasababisha Tamasha la Bruno Mars kufutwa

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tamasha la mwanamuziki kutoka nchini Marekani Bruno Mars lililopangwa kufanyika Tel Aviv, Israel usiku wa Jumamosi ya wiki iliyopita limefutwa baada ya vita kuibuka nchini humo.

Tamasha hilo ambalo ilikuwa ni la pili kwa Bruno kulifanya nchini humo baada ya lile la kwanza kufanyika siku ya Jumatano, ilikuwa imepangwa kuhudhuriwa na zaidi ya mashabiki 60,000.

Kitendo cha kughairishwa kwa tamasha hilo kimewanyima waandaji na waratibu wa kampuni ya Live Nation Israel zaidi ya tsh 75 bilioni ambazo walizikusanya kwenye mauzo ya ‘tiketi’.

Kwa mujibu wa ‘ripoti’ kutoka Business Insider tayari ‘tiketi’ zote ziliuzwa na kilichokuwa kinasubiriwa ni show tu kufanyika lakini baada ya machafuko kutokea tamasha hilo lilifutwa.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali ni kwamba ‘show’ hiyo ilikuwa inagharimu dola 500 kwa kiingilio cha chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live