Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vipimo mwili wa Mohbad vyakamilika

Ngoma 3 Za Mohbad Zaingia Kwenye 10 Bora Chati Ya Billboard.png Vipimo mwili wa Mohbad vyakamilika

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa aliyekuwa staa wa muziki nchini Nigeria, Ilerioluwa Oladimeji Aloba maarufu kama MohBad (26) umefanyiwa vipimo tayari kwa ajili ya kubaini chanzo cha kifo chake.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano kwa Umma wa Jeshi la Polisi Lagos, Nigeria, SP Benjamin Hundeyin amesema mwili wa Mohbad baada ya kufukuliwa ulichukuliwa sampuli na kupimwa (Autopsy/Post-Mortem).

SP Benjamin ameeleza mwamba majibu ya vipimo hivyo yatatoka hivi karibuni; "Jeshi la Polisi linapenda kuutaarifu umma kuwa taratibu za uchunguzi wa maiti (autopsy) ya Mr Mohbad umekamilika,” amesema SP Benjamin Hundeyin kupitia Twitter.

Kifo cha mwanamuziki huyu kilitokea katika mazingira ya kutatanisha Septemba 12 2023, ambapo mpaka sasa mwanamuziki Naira Marley amehusishwa na kifo hicho, ingawa yeye anadai hahusiki na anaungana na Watu wengine kuishauri polisi ifanye uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha staa huyo...

Si nchini Nigeria pekee ama Barani Afrika tu, bali kifo cha Mohbad kimegusa mpaka wanamuziki wakubwa nchini Marekani, wakiwemo Meek Mill, Lil Durk, Kodak Black.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live