Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Chadema wasomewa mashtaka nane (+video)

Video Archive
Wed, 28 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho,leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.



Viongozi wa Chadema wengine waliofikishwa Mahakamani hapo ni Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalim, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Ester Matiko Mbunge.

Hata hivyo viongozi hao baada ya kufika Mahakamani hapo wamesomewa mashtaka nane katika Mahakama hiyo ikiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwiline Bafta.

Katika mashtaka hayo, Mh. Freeman Mbowe anakabiliwa na mashtaka saba ambayo ni kufanya mkusanyiko usio halali, maandamano, kuhamasisha chuki na uchochezi wa Uhasi.

Katibu Mkuu,Dkt. Vicent Mashinji wanakabiliwa na makosa mawili ya kufanya maandamano na mkusanyiko usio halali, huku Msigwa akikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kushawishi raia kutenda kosa la jinai.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa serikali Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na kesi bado inaendelea mpaka sasa

Chanzo: bongo5.com