Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video ya binua ya Maua Sama yaiva

C7bf31f0d75f324a4806182e223e3714 Video ya binua ya Maua Sama yaiva

Sat, 19 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa Bongo Fleva, Maua Sama anatarajia kuachia video mpya ya wimbo alioachia hivi karibuni wa ‘Binua’.

Kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, nyota huyo aliyewahi kutamba na kibao cha Iokote inaonesha msanii huyo wa kike akiwa na mwongozaji wa video za muziki kwenye mazingira tofauti tofauti.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, alisema baada ya kuachia wimbo huo haitachukua muda mrefu kutoa video yake.

“Nimeachia wimbo wangu mpya wa Binua ni mzuri ambao mapokezi yake naamini yatakuwa makubwa kama nyimbo nyingine nilizoachia nyuma na sitachukua muda mrefu nitaachia video,” alisema.

Alisema video hiyo itakuwa ya kisasa akitumia mazingira tofauti na yale waliyozoea kutumia wasanii wengi wa nchini.

“Najua mashabiki wangu wanatarajia video bora itakayolingana na wimbo wangu na kikubwa siwezi kuwaangusha siku zote nafanya kazi ambazo zinafanya waendelee kufurahi na kuniunga mkono,” alisema Maua

Chanzo: habarileo.co.tz