Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vicky Kamata na Ferooz walijua kuzitendea haki siku za Wanawake na Ukimwi

Vicky Kamata Na Ferooz  Gf Vicky Kamata na Ferooz.

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Najua bado mnamalizia kiporo cha Siku ya Wanawake lakini sio mbaya japo kifupi tu tupige Soga kidogo, ujue wasanii ni kioo cha jamii kupitia tungo zao zinazoleta ushawishi kwenye jamii basi imekuwa kiungo muhimu katika kurahisha namna ya kufikisha ujumbe juu ya masuala mbalimbali kwani tungo hizo zina uwezo wa kujenga au kubomoa.

Muziki hupenya Moyoni na kuziteka hisia za mtu na ndio maana hata mamlaka zinawatumia wasanii katika shughuli zao mbalimbali.

Sasa kumekuwa na nyimbo zinazotungwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku mbalimbali lakini leo tutatazama zaidi zile ambazo zimepenya vilivyo kiasi cha kuishi masikioni mwa watu wengi huku zikiwa kama mpya kila siku pia zikiwapa ugali wasanii walioziimba mpaka kesho.

Nyimbo hizi ni ile ya Ferooz ya Starehe iliyokuwa ina maudhui juu ya Gonjwa hatari la UKIMWI lIlilokuwa limeshika kasi mwanzoni mwa miaka ya 2000 toka wimbo huo utoke zaidi ya miaka 15 iliyopita bado unaishi na kila ifikapo Disemba Mosi siku ya maadhimisho ya UKIMWI Duniani basi haiwezi pita siku hiyo bila kuusikia wimbo huo ukipigwa na hata kumpa shoo msanii husika ingawa kwa sasa hayupo sana kwenye masikio ya watu.

Si ajabu hata leo kama nikikuuliza kuwa ikiwa imefika Machi 8 ambayo ni siku ya Wanawake jaribu kusikiliza redio mbalimbali usipousikia wimbo wa Vicky Kamata 'Wanawake na Maendeleo' basi njoo unidai Milioni 1 najiamini kabisa lazima utausikia tu.

Lakini je kuna nyimbo ngapi zenye maudhui juu ya Wanawake lakini huu wa Vicky ambao ulitengenezwa katika Mazingira usiyotegemea Mhadhiri wangu mmoja wa SAUT Mwidima enzi akiwa bado mwanafunzi alitusimulia namna walivyoshoot na wakashangaa mzigo umekuwa mkubwa umeenda mjini kweli kweli na kumfungulia milango ya mingi Vicky akiwa bado mwanafuzi.

Ndio maana huu wimbo siku zote utabaki kuwa kileleni ni kama kule Ulaya wimbo wa All I want for Christmas is you wa Mariah Carey kila ifikapo Disemba huingia chati za juu ilihali unazaidi ya miaka 20.

Mwisho kabisa ifahamike kupata nyimbo kama hizi si uwezo wa msanii peke yake tu bali pia ni Baraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live