Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vera Sidika na mwigizaji Kate Actress washinda Tuzo Nigeria

Vera Sidika Na Mwigizaji Kate Actress Washinda Tuzo Nigeria Vera Sidika na mwigizaji Kate Actress washinda Tuzo Nigeria

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Sosholaiti Vera Sidika na muigizaji Kate Actress wameshabikia ushindi baada ya kuibuka washindi katika Tuzo tofauti za Wanawake mashuhuri Afrika 2023 tuzo ambazo zilipeanwa Nchini Nigeria.

Wawili hao walionyesha furaha yao kwenye mitandao yao ya instagram huku wakishukuru wote ambao waliwapigia kura kufanikisha ushindi huo.

Vera Sidika alisherehekea kwa kushinda tuzo ya Sosholaiti mashuhuri Afrika katika taji la tuzo za Africa Women Awards 2023 nchini Nigeria.

Sidika aliwashida waigizaji wanne wa Nigeria na kutwaa taji hilo,Sosholaiti huyo wa mwaka 2023 alitoa shukrani zake kwa kuwashukuru mashabiki wake kwa kumpigia kura.

"Asanteni sana kwa kila mtu aliyenipigia kura kunyakuwa tuzo hiyo,"aliandika kwenye Instagram.

Kwenye tuzo ya pili Mwigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress alishinda taji la Mwigizaji bora wa kike mwaka 2023 katika Tuzo za Wanawake wa Afrika. Kate alishindana na waigizaji tisa kutoka Nigeria, kuku akiibuka kama Mkenya pekee aliyeteuliwa katika kitengo hicho.

Akielezea furaha yake baada ya kutangazwa mshindi, Kate alitoa shukrani zake kwa mashabiki wake.

"Mmeamua ni wow! wow! wow! design ya ambulance mwaka mzima, Thank you Fam," Kate aliandika kwenye mtandao wake.

Chanzo: Radio Jambo