Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vera Sidika asherehekea miaka 10 ya umaarufu

Vera Sidika Mdqw Vera Sidika

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vera Sidika, mwanafasheni ambaye pia ni mwanasosholaiti mstaafu amejipiga kifua kuwa wiki kesho atasherehekea kudumu kwa miaka 10 kama mwanasosholaiti na mtu maarufu ambaye amekuwa akitajwa sana kwenye nyimbo za wasanii wa ndani na nje ya Kenya.

Sidika alikuwa akijibu swali la shabiki wake mmoja aliyetaka kujua jinsi anavyojihisi anapotajwa kweney ngoma za wasanii na kila mtu kumzungumzia mitandaoni.

“Huwa unajihisi aje wakati wasanii haswa kutoka Tanzania wanapokutaja kwenye mashairi yao ya ngoma,” shabiki alitaka kujua.

“Kusema kweli mimi ndiye mtu maarufu kutoka Kenya ambaye ametajwa sana kwenye ngoma za wasanii. Nimekuwa maarufu kwa miaka 10 na mnamo Desemba 17, nitasherehekea miaka 10 ya kuwa maarufu,” Sidika alisema.

Alisema tarehe hiyo pia itakuwa kumbukumbu ya kusherehekea ndoa ya wazazi wake huku akisema ni kama ujauzito wake ulitungwa Desemba ya mwaka 88 na umaarufu wake ukaanza tarehe kama hiyo lakini mwaka tofauti.

“Hii pia itakuwa kumbukumbu ya harusi ya wazazi wangu, ni kama ujauzito wangu ulipatikana Desemba 17 mwaka 1988, nikazaliwa miezi 9 baadae na umaarufu ukaja tu tarehe na mwezi sawia, mwaka tofauti,” Sidika alitamba.

Mama huyo wa mtoto mmoja pia alifutilia mbali uvumi kuwa yuko mjamzito tena na kusema kwamba yeye anamshughulikia bintiye Asia Brown kuanza shule mwaka kesho Januari.

Asia Brown miezi michache iliyopita alikuwa anasherehekewa na wazazi wake Vera Sidika na Brown Mauzo kufikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live