Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vera Sidika aonesha mfuko wake wenye thamani ya nusu milioni

Vera Sidika Aonesha Mfuko Wake Wenye Thamani Ya Nusu Milioni Vera Sidika aonesha mfuko wake wenye thamani ya nusu milioni

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasosholaiti Vera Sidika amerejea nchini baada ya ziara yake ya miezi miwili marekani na kusimulia furaha yake kwa kufanikiwa sana katika matangazo ya biashara katika nchi za nje.

“Nina furaha kurejea nchini,ninafurahia kuwa mbali kwa sababu ninaweza kufanya mambo yangu ninavyotaka ,nchi za nje zimenawiri sana kimapato na mimi kufanya kazi zangu huko nifuraha tele", alisema Vera.

Katika mahojiano na wanablogu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumapili, Oktoba 15, Vera alionesha mfuko wake wenye jina Christian Dior ambao alidai ni wa dhamani ya zaidi laki tano pesa za Kenya.

Vera Sidika ni mama wa watoto wawili na mmoja wanasosholaiti wenye wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii. Anajulikana kwa maisha yake ya kifahari kwa kununua bidhaa zenye bei ghali.

Waliomulaki Vera walikuwa kaka yake, Josh, na binti yake, Asia Brown.

Vera alitoa shukrani zake kwa familia yake kwa kujitokeza kuwaangalia watoto wake alipokuwa katika ziara yake ya miezi miwili.

Alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na aliyekuwa na mpenzi wake Brown Mauzo alijibu kwa ghahabu na kutangaza kutojishirikisha naye katika maisha yake.

“Sitaki kumuona Brown Mauzo popote karibu yangu,Nijuavyo, tumeachana naye kwa amisha yangu sitaki kujishugulisha naye vyovyote vile",alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live