Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vera Sidika afanyiwa upasuaji, kalio lote lapukutika

VERA ZAMANI NA SASA Vera Sidika afanyiwa upasuaji, kalio lote lapukutika

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo maarufu kutoka nchini Kenya, Vera Sidika, ameeleza kuwa, amelazimika kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kujinusuru afya yake baada ya awali kufanya upasuaji wa kutengeneza shepu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera ameposti picha mpya inayomuonesha akiwa hana lile kalio lake na kueleza hivi:

Hii imekuwa awamu ngumu zaidi maishani mwangu, kwa sababu ya hatari na matatizo ya kiafya , ilinibidi kufanyiwa upasuaji.

Bado haiaminiki sana lakini nimekubali na nimejifunza kujipenda bila kujali. Wanawake; pls jifunze kujipenda & usiwahi kuruhusu shinikizo la rika likuharakishe katika mambo yatakayokuharibia siku zijazo.

Nimebahatika kuwa hai, Mungu ananipenda sana. Kusema kweli imekuwa ngumu sana, hata sikusherehekea siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu, lakini hapa tumefikia. Heri ya kuzaliwa kwangu.

Mpya mimi. Nimekuja kuthamini maisha na kamwe sichukulii mambo kuwa ya kawaida. Asante kwa familia yangu, haswa mume wangu kwa kuwa karibu nami.

Kwa mashabiki wangu: Mimi bado ni mrembo yule yule Vera Sidika na hilo halijabadilika. Nakushukuru kwa upendo & support & kuomba utapitia safari hii pamoja nami.

Nitakuwa nikiweka video zangu za safari ya upasuaji hapa, kwa wale ambao wamekuwa wakifikiria kupata upasuaji wa kuongeza makalio au kubadilisha chochote kwenye miili yao hii inaweza kubadilisha mawazo yako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live