Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vazi la vijiko la Harmonize laibua gumzo

74683 Harmonizepic Vazi la vijiko la Harmonize laibua gumzo

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Vazi la vijiko alilolivaa msanii wa Bongofleva, Rajab Abdul maarufu Harmonize katika wimbo wake mpya wa Attitude aliouachia siku nne zilizopita na kuwasharikisha wasanii Awilo  Longomba kutoka Jamuhuri ya Kongo na H.Baba kutoka Tanzania laibua gumzo. Harmonize aliweka picha ya vazi hilo leo Jumanne Aprili 27,2021 katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ukimuonyesha kavaa koti jeusi lililoning’inia vijiko, umma na visu. Baadhi walioina picha hiyo walitoa maoni yao akiwemo Ibrah_Darasa ameandika ”Yani hapo ukifika kwa hoteli hamna kusumbuka. Pilly Rajabu ameandika ”Jamani ni nguo au kabati la vyombo wakati Suluma56's ameandika “Mmakondeee katika ubora wake vijiko Kariakoo viatauzwa elfu kumi. Tin thony ameandika ”Sherehe yoyote tunavamia bila tabu... set up tayar tunayo..Hii fashion kiboko...vyombo vitaisha. Kwa upande wake Tzswag ameandika ”Hotel management jacket huku Kikoti Junior, ameandika “Kama washing machine haiwezi fua hiyo kitu dobi si ndio anaweza pata ukilema kabisa akijaribu kukufulia ,”. Naye Janempaka ameandika ”Hakikisha nyimbo nyingine unavaa sufuria."

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz