Mwimbaji wa Bongofleva, Vanessa Mdee amedokeza kurejea kwake tena katika muziki ikiwa ni miaka miwili tangu kutangaza kuacha muziki.
Utakumbuka Julai 2022 Vanessa Mdee alitangza kuachana na muziki kwa madai ya kutomlipa na kumsababishia msongo wa mawazo.
Hivi karibuni Vanessa Mdee alichapisha video ya kumbukumbu alipokuwa akitumbuiza kwenye Jukwaa la Crans Montana mwaka 2019.
“Namiss kutumbuiza, naamini Mungu kwa hatua yangu inayofuata kama mtumbuizaji, nasubiri maagizo yake.” alisema Vanessa.
Ikumbukwe baada ya Vanessa Mdee kuacha muziki amejaliwa watoto wawili na Mchumba wake, Rotimi ambaye wanaishi wote nchini Marekani.