Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vanessa Mdee azindua ‘app’ yake Vee Money

1592 Screen Shot 2018 01 19 At 16.32.57.png TZW

Fri, 19 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki, Vanessa Mdee anayefanya vizuri katika soko la muziki nchini Tanzania ameendelea kuwa na wiki ya kihistoria ambayo ilianza kwa kuzindua albamu yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake na wadau wengine wa mziki nchini siku ya Jumatatu.



Vanessa Mdee

Ijumaa hii Vanessa amezindua programu ‘app’ yake mpya ya simu ya VEE MONEY ambayo inapatikana bure kupitia ‘Google Play store’ na ‘Apple store’. Programu hii ambayo imetengenezwa na kampuni ya masuala ya teknolojia ya Marekani, Converge Media, ni sehemu ambayo mashabiki wa Vanessa watakuwa wanapata maudhui ya kipekee ya Vanessa kama vile; nyimbo, video, picha, na kuona kurasa zake za kijamii.



‘Kwanza natoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea albamu yangu kwa mikono miwili, na sasa natumaini app hii itazidi kutuweka karibu,” alisema Vannesa.

Vanessa atakamilisha wiki yake ya kihistoria kesho kwa kuweka sahihi katika albumu zake tukio ambalo litafanyika eneo la Mlimani City Mall kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Chanzo: bongo5.com