Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vanessa Mdee amekuwa msanii wa kwanza Afrika kupata dili hili

368 Screen Shot 2017 12 19 At 12.32.23 PM 601x400.png TZW

Tue, 19 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Staa wa muziki Vanessa Mdee ni miongoni wa wasanii wa Tanzania wanaoutambulisha vyema muziki wa Bongo Fleva kimataifa, kutokana na juhudi ya kazi zake anazofanya ameamua kutupa habari njema ambayo itakuza muziki wa bongofleva kupitia mtandao wake wa instagram baada ya kupata dili  Universal Music Group yaMarekani.

Baada ya kupata shavu hilo lenye mkwanja mrefu ameamua kuandika caption inayowashukuru mashabiki na watu wake wa karibu “Kama ilivyo ada, tunaanza kwa kumshukuru mwenyezi mungu kwa baraka zake na kibali chake cha kutufikisha siku njema ya leo Nawashukuru mashabiki wangu, ndg, jamaa na marafiki wa karibu, tuliokuwa sambamba tangu mwaka unaanza mpaka hivi sasa tukielekea ukingoni”

“Nimeona niitumie siku na fursa hii kuwajulisha wapendwa mashabiki zangu, Mwanzoni mwa mwaka huu, Nilipitia changamoto nyingi Sana Lakini kwa neema za Mungu , Nilitoka mahali pale na sio kuona baraka tu bali na maajabu mengi yaliyotokea kwenye maisha yangu”

“Ikiwemo kuwa mmoja wa familia ya Universal Music Group in a unique joint signing between @universalmusicgermany@airforce1 na @universalmusicgroup na hii ni mara ya kwanza kwa Msani wa Kiafrika kupata deal ya aina hii yenye mkwanja mrefuuuuuuuuuuu sana

Chanzo: millardayo.com