Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vanessa Mdee afanyiwa Oparesheni ya Jicho (+Video)

Gfftcgftfg Vanessa Mdee afanyiwa Oparesheni ya Jicho

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva nchini ambaye kwasasa anaishi Marekani na mpenzi wake Rotimi ameweka wazi kuwa amefanyiwa upasuaji (Surgery) wa jicho na kuwa kwa sasa anaendelea vizuri.

Vanessa ameweka wazi suala hilo kupitia ukurasa wake wa #TikTok kwa ku-share video akiwa na #Rotimi wakicheza kwa furaha huku video hiyo ikiwa na maandishi ya kumshukuru mungu kwa upasuaji wake kwenda salama.

Utakumbuka kuwa mwaka 2019 Vanessa aliweka wazi kuwa jicho lake moja linashida ya kutokuona hivyo amekuwa akitumia jicho moja kwa takribani miaka sita.

#VanessaMdee aliweka wazi suala hilo wakati alipokuwa Jaji kwenye mashindao ya ‘East Africa Got Talent Show’ 2019 alipokuwa akimtia moyo mshiriki aliyuekuwa na matatizo ya macho.

Vanessa Mdee ‘#VeeMoney’ amewahi kutamba na vibao vyake kama ‘Cash Madame’, ‘Juu’, ‘Come Over’ ‘#Kisela’ na nyinginezo.

View this post on Instagram

A post shared by Mwananchi Scoop (@mwananchiscoop)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live