Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Zuchu afunguka

Zuchu+1+pic VIDEO: Zuchu afunguka

Thu, 24 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By NASRA ABDALLAH ASIKUAMBIE mtu, licha ya uchanga wake kwenye tasnia ya muziki, lakini kwa muda mfupi tangu atambulishwe mwimbaji chipukizi kutoka WCB, Zuchu amefunika kinoma.

Mwanadada huyo ambaye majina yake kamili ni Zuhura Othman, mtoto wa nyota wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Omar Kopa amejizolea umaarufu mkubwa na kupata wafuasi wengi kwa muda mfupii, ikiwa ni miezi minne tu tangu atambulishwe katika lebo ya WCB.

Achana na ngoma zake tisa zilizopo kwenye EP yake iitwayo ‘Am Zuchu’ aliyoiachia Aprili mwaka huu, lakini Zuchu amekuwa midomoni mwa watu hasa ukaribu wake na Diamond na naona nyota yake ilivyong’ara ghafla na kuna baadhi hawamjui kwa undani mwimbaji huyo.

Hata hivyo, Mwanaspoti limepata wasaa wa kufanya mahojiano maalum naye nyumbani kwa bosi wake, Diamond Platnumz maeneo ya Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam na kufunguka mambo mengi kuhusu yeye na mipango yake kimuziki. Ebu endelea naye upate uhondo kamili.

HUBEBA NINI KATIKA POCHI

Kama mastaa wengine wa kike huwa hawaachi pochi katika mitoko yao, Zuchu alipoulizwa kitu gani hakikosekani kwenye pochi lake, mwanadada huyo anakiri ukiacha vitu vingine, hawezi kutoka nyumbani bila kubeba dawa ya kupunguza athari ya Ugonjwa wa Pumu iitwayo inhaler.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz