Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#VIDEO: Unataka kuifahamu muvi mpya ya Uwoya Olema? Hii hapa...

Irene Uwoya Unataka kuifahamu muvi mpya Olema? Hii hapa...

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama unataka kuifahamu kwa ufupi filamu mpya ya muigizaji Irene Uwoya, mtangazaji Millard Ayo ameielezea kwa ufupi kupitia Instagram yake.

Millard ameposti kipande cha video(trela) na kisha kuandika hivi:

Kabla sijasema chochote naomba kwanza niweke wazi kwamba nimekua shabiki mkubwa wa mwigizaji Irene Uwoya kwa miaka mingi sana kwa hiyo ile kiu yangu ya miaka mitano bila kutazama movie yake aliyosimama yeye kama yeye hatimaye inakwenda kumalizwa kesho hapa Arusha kwenye uzinduzi wa hii movie yake mpya iitwayo OLEMA.

Kwenye maongezi yangu na Staa huyu usiku huu ameniambia maana ya OLEMA ni kafara, pili story yake ni ya Mwanamke mmoja aliyekua ameolewa na Mwanaume Tajiri na Mafya wa Arusha lakini baada ya manyanyaso kuzidi akashindwa kuvumilia na kuamua kutimkia kusikojulikana.

Siku aliyomtoroka Mumewe ndio siku Mwanaume huyo alirudi nyumbani na vitu vyenye thamani ambavyo Mke huyo aliamua kuviiba akaanze maisha sehemu nyingine, hapo ndio tatizo lilipoanzia kwani vitu hivyo havikua vya Mumewe bali vya Mataita wengine wenye roho mbaya ambao waliishia kumuua Mume na kuanza kumsaka Mwanamke huyo ambaye mwisho wa siku alijikuta amekimbilia umasaini.....na huko umasaini nako pakawa pazito.....

Irene ameniambia ana mpango wa kuizindua movie hii kwenye mikoa mbalimbali ukiachia hiyo ya Arusha kesho na kisha baadaye ndio atatangaza wapi Mashabiki wanaweza kuitazama ikiwemo mitandaoni.

View this post on Instagram

A post shared by Irene Uwoya (@ireneuwoya8)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live