Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: TAMTHILIA YA SULTAN: Salum Said anayeigiza Taslican anayeghan mashairi

Video Archive
Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Taslicali

Taslicali Yahya Bey ni mtunzi na mwimbaji (ana ghani) mashairi. Katika tamthilia hiyo anaigiza kama mlinzi wa Shazad Mustafa.

Salum Said

Kitaaluma ni mpiga picha ambaye sasa amekuwa mghani mashairi akiwa Taslicali Yahaya wa Tanzania.

Salum anasema anafurahi kuifanya kazi hiyo, kwa kuwa ameshaifanya kwa muda mrefu ikiwemo katika michezo ya redio na matangazo.

Ameshiriki katika michezo mbalimbali ya televisheni na redio ikiwamo Mambo Bomba, Wahapahapa, Kizazi Njia Panda kipindi kinachorushwa katika shirika la Habari la Sauti ya Ujerumani (DW).

Katika tamthiliya hiyo, Yahaya anampa mashairi ya nguvu mtoto wa Sultan ambaye anampenda.

Kati ya vitu vinavyomuudhi anasema ni pale anapojikuta mtoto huyo wa kike anakaribia kuingia kwenye 18 zake, halafu wanatokea walinzi kumuita na hivyo kukatisha zoezi hilo.

Anaeleza kuwa anashukuru nafasi anayoicheza inapendwa na watazamaji kwani hata anapokuwa kwenye mkusanyiko watu huanza kumsifu.



Chanzo: mwananchi.co.tz