Kikao kati ya baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na msanii Rayvanny kimeonekana kuwa kizito baada ya mameneja wawili wa lebo ya WCB kuingia muda huu kwa kile kinachoonekana kuongeza nguvu.
Mwandishi wa MCL Digital aliyepiga kambi katika ofisi za Basata zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam, amewashuhudia mameneja hao Babu Tale na Mkubwa fela wakiwasili saa mbili baada ya kikao kati ya msanii huo kuwa tayari kimeshaanza.
Wakati Babu Tale aliwasili saa 7:19 mchana, Mkubwa Fela aliwasili saa 7:28 na kuungana na kina Rayvanny katika mahojiano na baraza hilo katika ofisi ya Katibu wake, Godfrey mngereza.
Baada ya kuingia vigogo hao walitoka nje ya chumba cha ofisi hiyo na kuanza kujadiliana wenyewe kwa zaidi ya dakika 20.
Anahoji, “inakuwaje bomba la mafuta ya hazina iliyoko ardhini iliyojengwa na serikali iishie kuwa chini ya uendeshaji wa mtu binafsi?”