Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO:Piere avamia meza ya majaji BSS, akalia kiti cha jaji mkuu

89893 PIERREPIC VIDEO:Piere avamia meza ya majaji BSS, akalia kiti cha jaji mkuu

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya ukimya mrefu, mchekeshaji Piere Liquid ameibukia kwenye shindano la Bongo Star Search (BSS) na kuvamia meza ya majaji.

Piere hivi karibuni alijikuta akipata umaarufu kupitia vibwagizo vyake kama utabaki kileleni, mama nakufaa, chiii, hiyooo !!.

Kutokana na hilo alijikuta akipata mialiko ikiwamo kwenda bungeni na kualikwa kuwa mgeni maalum katika matukio mbalimbali ya burudani.

Hata hivyo usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 25, 2019, katika fainali za mashindano ya Bongo Star Search (BSS), zilizofanyika ukumbi wa Next Door Arena, Dar es Salaam alionekana kuwa kivutio hasa pale alipovamia meza ya majaji wa shindano hilo na kukaa.

Piere alifanya tukio hilo saa 6:45 usiku baada ya jaji mkuu wa BSS, Rita Paulsen kwenda jukwaani kwa ajili ya kumtangaza mshindi.

Mchekeshaji huyo ambaye alikuwa kavaa shati na kaptura ya kitenge, ghafla alionekana kapanda kwenye meza ya majaji ambapo Dully Sykes ambaye alikuwa mmoja wa majaji alimshika mkono na kumsogezea kiti alichokuwa amekaa Rita.

Pia, Master Jay aliyekuwa mezani hapo naye alimpa ushirikiano kwa kuongea naye huku akionekana kumwelekeza kuweka chini ya meza kinywaji alichokuwa anakunyw, hali iliyotafsiriwa ni kuogopa kukitangaza kutokana na kuwapo kwa kinywaji kilichodhamini mashindano hayo.

Pamoja na ukarimu huo, Piere hakuweza kutulia kwani baada ya Rita kumtangaza mshindi ambaye ni Meshack Fukuta kutoka mkoani Mbeya, aliwaacha akina Master Jay na Dully na kwenda kupanda jukwaani ambapo watu walikuwa wakimshangalia.

Hata hivyo, hali hiyo ilitulizwa na walinzi maalum waliokuwa wakimlinda Rita kwa kwenda kumshusha jukwaani Piere ili kupisha shughuli zingine ziendelee ikiwamo za wageni mbalimbali kupiga picha na mshindi na washiriki wa shindano hilo. 

Chanzo: mwananchi.co.tz