Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#VIDEO: Penzi na Paula na Marioo halitafika Disemba - Baba Levo

#VIDEO: Penzi Na Paula Na Marioo Halitafika Disemba   Baba Levo #VIDEO: Penzi na Paula na Marioo halitafika Disemba - Baba Levo

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chawa wa WCB Wasafi mwenye domo kama tarumbeta Baba Levo ameibuka na madai mapya kuhusu uhusiano wa msanii Marioo na binti wa muigizaji Fridah Masanja, Paula.

Akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni, Baba Levo alikiri tena bila kupepesa jicho kwamba penzi la wawili hao ambalo limekuwa likitajwa kama kiki halitofika mwezi Desemba mwaka huu.

Akitetea maoni yake, Baba Levo alisema kuwa vitatokea viwili kupelekea penzi lao kusambaratika kabla ya tamati ya mwaka.

“Penzi la Marioo na Paula halitofika mwezi wa kumi na mbili. Ni vitu viwili, ama Marioo atakuwa ameishiwa hela kabisa na kuwa ombaomba, au ndugu yetu [Paula] atapata mtu mwingine mwenye hela Zaidi,” alisema akiashiria kwamba huenda Marioo anachunwa kushoto kulia na kibubu chake cha hela kimekuwa chepesi.

Baba Levo ambaye ni mtetezi mkali wa sera za WCB Wasafi alisema kuwa ana ushahidi wa jinsi Paula na mama yake walivyo na historia ya unyonyaji wa mali za mwanamume anayekanyaga kwenye anga zao akisema aliliona hilo hata katika Rayvanny kipindi Paula wanachumbiana naye.

“Niliona Rayvanny kuna muda alikuwa anaendesha gari akiongea peke yake. Kwa namna ambavyo alikuwa ameshapigwa mizinga, unapigwa mzinga huku chini unapigwa juu unapigwa kushoto unapigwa kwa mama, mtoto anakushambulia,” Baba Levo alisema.

Alisema eti Rayvanny kwa kipindi kimoja ilibidi amfuate na kumuomba ushauri akisema kuwa nusra alikuwa afe kutokana na msongamano wa mahitaji ambayo alikuwa anatakiwa kutekeleza kwa Paula na mama yake.

“Aliniambia huku naona nitakufa Baba Levo, huku naombwa sijui chuo, huku sijui hela ya habaya… alibaki hpi, alichanganyikiwa,” alisema.

View this post on Instagram

A post shared by Emanuel Msigwa (@swahiliwaves)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live