Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#VIDEO: Nay wa Mitego aitwa Central 'siogopi hata nikilala wiki'

Nay Wa Mitego 2 #VIDEO: Nay wa Mitego aitwa Central 'siogopi hata nikilala wiki'

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapper Nay wa Mitego amewasili katika kituo cha Polisi Kati (Police Central) jijini Dar es salaam kuitikia wito kuhusu wimbo wake wa ‘Amkeni’ ambao hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuufungia kuchezwa katika vituo vyote vya Radio na Televisheni.

Nay ambaye amewasili akiwa na Mwanasheria wake Jebra Kambole amenukuliwa akisema "Ukiwa sauti ya Watu kuja sehemu kama hii ni kawaida, mimi ni sauti ya Watu acha nikawasikilize nitakuwa na cha kuongea lakini kwa sasa sina, nimeambiwa tu ni wimbo wangu wa 'Amkeni' kwa hiyo nataka nikajue umefanya nini, kuna tatizo gani."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live