Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mwili wa msanii wa muziki Tanzania Mbalamwezi kuzikwa mapema kutokana na kuharibika

Video Archive
Fri, 16 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwili wa msanii wa muziki nchini Tanzania, Abdallah Matimbwa maarufu ‘Mbalamwezi’ utazikwa kesho Jumamosi Agosti 17,2019 kabla ya saa 6 mchana.

Ally Mponda ambaye ni mjomba marehemu akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Agosti 16,2019  amesema hatua ya kuamua kuuzika mwili huo mapema unatokana na kuharibika.

Mponda amesema maziko hayo yanatarajiwa kufanyika kati ya makaburi ya Kamla au Kilimahewa yaliyopo Tandika Jijini Dar es Salaam.

 "Tumemuona Dula ameharibika sana, hivyo tusingependa kuuweka mwili wake muda mrefu, inawezekana tukamzika saa nne na tumechelewa sana haitazidi saa sita," amesema Mponda.

 Akielezea kuhusu taarifa za kupotea kwake, amesema marafiki zake wamesema hawakumuona tangu sikukuu ya Iddi na hii ni baada ya kumuacha kwenye nyumba wanayoishi na wao kwenda zao kwenye shoo.

Siku hiyo, amesema Mbalamwezi alikataa kwenda na wenzake na kubaki nyumbani lakini baadaye waliporudi hawakumkuta.

Habari zinazohusiana na hii

"Baada ya kuona mwenzao hajarudi walipiga simu bila ya kupokelewa na kulipokucha wakaanza kumtafuta, mpaka wanapata taarifa za kifo chake katika kituo cha Polisi siku nne zilikuwa zimepita. Kufuatia hali hiyo jana  usiku wakaja kutoa taarifa kwa  ndugu,” amesema mjomba huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz