Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mfahamu Ramla Abdul anayeigiza Kiswahili sauti ya binti wa Sultan

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ni tamthilia inayohusu maisha ya Sultan Suleyman. Katika umri wa miaka 26 alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottomans akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great. Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim…

Kuhusu Mihrimar

Nafasi ya Mihrimar katika tamthilia hii imeigizwa na watu watatu ambao ni Ayda Acar, Melis Mutluc na Pelin Karahan. Kwa maana hii Mtanzania, Ramla anayetafsiri nafasi hiyo anawakilisha watu watatu tofauti. Mihrimah ni mtoto wa pekee wa Sultan Suleyman na Hurrem Sultan. Pia ni mke wa  Rustem Pasha.

Mmoja wa waigizaji waliocheza nafasi kubwa katika nafasi hiyo ni Pelin Karahan ambaye ni mwanamitindo na mtangazaji wa televisheni maarufu nchini Uturuki.

Amejizoea umaarufu kwa kucheza tamthilia nyingine maarufu za Kavak Yelleri, Mavi Kelebekler na Yeter.

Ramla Abdu (Mihrimah)

Ni mwalimu aliyechukua wiki mbili kujifunza kumnakili Mihrimah kwa Kiswahili.

Ramla anasema alikuwa akipenda kufanya kazi hiyo kwa sababu ya kuwa na tabia ya kufuatilia filamu nyingine zilizokuwa zimetafsiriwa.

“Yaani nilipoanza kazi hii hapa Azam, nilikuwa nakosea mara kwa mara jambo lililonichukua wiki mbili kuwekwa sawa na ninashukuru sasa nimetoka katika nafasi ya wahusika wadogo wadogo,” anasema.

Katika nafasi anayonakilisha kwa sasa ni Mihrimah ambaye ni mtoto wa Sultan.

Ili kujisahihisha kwa kazi aliyoifanya anasema amekuwa akirudi nyumbani mapema ili kuiangalia tamthilia hiyo kama moja ya njia ya kujifunza zaidi.



Chanzo: mwananchi.co.tz