Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mashabiki Dodoma wasubiri kwa saa 15 kumuona Diamond

Video Archive
Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mashabiki wa Diamond mjini Dodoma wamelazimika kwenda kwenye dirisha la chumba alicholala Diamond kwa lengo kutaka atoke kuwasalimia baada ya kumsubiri kwa zaidi ya saa 15.

Diamond ametumia treni kwenda Kigoma pamoja na mashabiki na familia yake kwa ajili ya kusheherekea miaka 10 ya kuwa katika muziki.

Kutokana na ratiba ya awali ya treni hiyo aina ya Deluxe, kutakiwa kuondoka saa 12:00 asubuhi ilishindwa kufanya hivyo na badala yake iliondoka saa 2:05 asubuhi.

Katika stesheni mbalimbali alizopita Diamond aliwapungia wananchi waliokuwa wanamsubiri kumuona na kati ya vituo alivyosalimiana na wananchi ni pamoja na ile ya Kidatu na Morogoro.

Katika stesheni ya Dodoma hali ilikuwa tofauti kwani treni hiyo iliyokuwa na abiria wengine wa kawaida wapatao 700 ilifika saa 3:00 usiku.

Baada ya kuwasili Dodoma mashabiki wake wa eneo hilo walimuita majina mbalimbali ikiweno Baba Lao, Simba na Diamond na kumuomba atoke nje awamsalimie japo kwa dakika chache.

Mkazi mmoja alisikika akisema"Huyu tumuimbieni kwa nguvu atatoka tu,"lakini pamoja na kufanya jitihada hizo wakiwa wamjikusanya zaidi ya 20, Diamond hakuweza kutokea kuwasalimia hata kwa kupunga mkono kama alivyofanya kwa maeneo mengine alikokwishapita.

Chanzo: mwananchi.co.tz