Msanii wa Bongofleva, Esterlinah Sanga, amesema kama Mungu atamjalia angependa awe na watoto watatu.
Akizunguma na MCL Digital hivi karibuni, Linah maarufu kwa jina la n’dege mnana’, kwa sasa tayari ameshapata mtoto mmoja aliyempa jina la Tracy Paris.
“Kiukweli tangu nimempata mtoto wangu nimeona raha sana ya kuitwa mama, na nina hamu ya kuwa na watoto zaidi ya huyu na Inshaallah Mungu akipenda basi walau watatu,”amesema.
Kuhusu kurudi kwake kwenye muziki, Linah amesema mashabiki watarajie ngoma tatu ndani ya mwaka huu.
“Linah ni yuleyule kwani ngoma yangu ya mwisho kuitengeneza niliifanya nikiwa mjamzito hivyo hakuna kilichobadilika,” amesema
Akiongelea suala la ujio wa wasanii wapya, Linah amesema haimpi shida zaidi ya kumuongezea hamasa ya kufanya vizuri.