Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Hassan Naseeb anayeigiza sauti ya mtoto pekee wa Sultan wa Mahidevran

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Sehzade

Mustafa

Nafasi ya Sehzade Mustafa ambaye ni mtoto wa sultan, imechezwa na watu watatu ambao ni Yusuf Berkan Demirbag, Tunc Oral na Mehmet Gunsur.

Aliyecheza nafasi kubwa katika nafasi hii ni Yusuf Berkan Demirbag, mwigizaji wa Kituruki ambaye alijizolea umaarufu kupitia filamu ya Can iliyotoka mwaka 2011.

Hassan Naseeb

Hassan Naseeb mzaliwa wa mkoani Morogoro, anasema mbali ya kunakili sauti kwenye Sultan, pia ananakili kwenye tamthiliya nyingine inayoonyeshwa mwishoni mwa juma ikiwemo ile ya ya Nagin na anajulikana kwa jina la Rock.

Kitaaluma anasema yeye ni mpigaji picha mzuri na ni muaandaaji wa vipindi vya tv ambako katika tamthilia ya Home Kweyu inayorushwa TBC yeye ndiye muongozaji.

Naseeb anasema malengo yake katika kuingiza sauti ni kufika mbali na anashukuru Azam kumpa nafasi hiyo huku akieleza waongozaji wa kunakili tamthilia hiyo wamechangia wao kuwa hapo walipo.

Akilinganisha Bongo Movie na tamthiliya hiyo, anasema alichokiona japokuwa hana muda mrefu katika tasnia hiyo ni kulipua kazi na hii inachangiwa na kuwa na bajeti ndogo.

Anasema wanapaswa kuingia katika mitandao kuangalia wenzao wanavyofanya ili nao waendane na soko linavyotaka badala ya kumtafuta mchawi.



Chanzo: mwananchi.co.tz