Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Godzillah aacha vilio kila kona

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanamuziki wa Hip Hop, Golden Mbunda maarufu Godzilla aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo ameacha simanzi kwa wasanii wenzake ambao kupitia mitandao ya kijamii wameelezwa namna alivyowagusa enzi za uhai wake.

Godzillah atakayekumbukwa kwa vibao vyake Nataka na Kingzillah amemwagiwa sifa na watu mbalimbali kwamba alikuwa na kipaji cha hali ya juu.

Mwanamuziki aliyewahi kushirikiana naye katika wimbo First Class, Mwasiti amesema kifo cha Godzillah kimemuachia maumivu makali

“Ooh GOD   umetangulia zizi jamani! Nipo kwenye maumivu makali mno! Mwenyezi Mungu naomba akupumzishe kwa amani kwenye nyumba yako ya milele Bestie. ’’

Mwanamuziki Shetta naye ameeleza hisia zake akiandika : ‘’ Sad (huzuni)  pumzika kwa amani Kingzillah Tutakukumbuka Daima milele Bro. Mungu akulaze mahali pema peponi Ameen’’

Malkia wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee mapema aliandika katika mtandao wa Instagram akiambatanisha na picha ya pamoja na mwanamuziki huyo huku akiacha ujumbe wenye mafumbo akisema:  “Hatukumtupa tulijaribu kuwa karibu naye na Kumbe ndio lilikuwa tabasamu la mwisho. Rest Easy Young bro @kingzilla tz.”

Ujumbe huo wa Lady Jay Dee uliibua maswali iwapo kulikuwa na kitu cha ziada kilikuwa kikimsumbua rapa huyo.

Vanesa Mdee naye aliandika ‘’Rest Easy King. Happy we lived to witness your greatness. May your legacy live on Baba Shwash. (Pumzika kwa amani mfalme. Tunashukuru tumeishi kuona uwezo wako. Kumbukumbu zako zitabaki nasi daima).’’

 

Soma Zaidi: VIDEO: Dada wa Godzilla asimulia rapa huyo alivyohangaika kabla ya kufikwa na umauti



Chanzo: mwananchi.co.tz