Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Gabo Zigamba afikisha tuzo nane za filamu

Video Archive
Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii Ahmed Salim’Gabo Zigamba’ amesema baada ya kutangazwa kuwa msanii bora wa kiume katika tuzo za Zanzibar International Film Festival (ZIFF) mwaka 2018 atakuwa sasa na jumla ya tuzo nane.

Baadhi ya tuzo ambazo amewahi kupata kama mwigizaji bora wa kiume ni Tuzo za filamu Tanzania(TAFA) zilizofanyika Aprili 2018,  za ZIFF mwaka 2017  na Tuzo za kituo cha Televisheni cha East Afrika mwaka 2016, Action and Cut zote katika filamu ya ‘Bado Natafuta’

Pia alishawahi kushinda kupitia filamu ya Siri ya Giningi na Safari ya Gwalu zilizoshinda kama sinema bora katika tuzo za filamu za nchini Rwanda.

Akizungumza na MCL Digital hivi karibuni, Gabo amesema, kuendelea kupata tuzo hizo kunampa hamasa ya kufanya kazi nzuri zaidi ambapo Jumamosi ya wiki hii anatarajia kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Sumu.

Amesema kinachomfurahisha zaidi katika tuzo nyingi alizoshinda anang’aa katika kipengele cha muigizaji bora wa kiume.

“Hata mwaka jana katika tuzo hizo za ZIFF nilishinda kipengele hicho kupitia filamu ya Gwalu na mwaka huu  kupitia filamu ya ‘In Segere’,” amesema

Hata hivyo wakati wa utopaji tuzo hizo, Gabo hakuwepo eneo la tukio, ambapo amesema ilitokana na yeye kuwa na majukumu mengine yaliyomlazimu kwenda Dar es Salaam japo alikuwa katika tamasha hilo kuanzia siku ya kwanza.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz