Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#VIDEO: Diamond alivyorudia nguo aliyoivaa miaka 4 iliyopita

Diamond Mtv #VIDEO: Diamond alivyorudia nguo aliyoivaa miaka 4 iliyopita

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka nchini #DiamondPlatnumz ameweka wazi kuwa koti alilolivaa katika wimbo wake ‘Tetema’ ndilo hilo hilo alilolivaa kwenye wimbo wa Komando alioshirikishwa na G Nako.

Diamond kupitia InstaStory yake ameandika kuwa,

“Nikuibie siri tu kuwa koti nililovaa kwenye ‘Komando’ ndiyo koti lile lile nililovaa zamani kwenye video ya ‘Tetema’, hii inaitwa utunzaji na kuheshimu mali, kiufupi kutotumia hela hovyo.”

Video hiyo ya 'Komando' imeachiwa siku jana Novemba 14, kwenye digital platform za msanii G Nako, hadi sasa tayari imefika number one trending YouTube. Huku video ya 'Tetema' ilitoka miaka minne iliyopita na hadi sasa imefikisha watazamaji zaidi ya milioni 77 kwenye mtandao wa YouTube.

View this post on Instagram

A post shared by Mwananchi Scoop (@mwananchiscoop)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live