Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: BSS 2019 yawakutanisha Jumanne Idd,Kayumba, Kala Jeremiah na Angelmary jukwaa moja

Video Archive
Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Fainali za mashindano ya Bongo Star Search (BSS), 2019 zimemalizika huku zikiwakutanisha mastaa mbalimbali waliowahi kupita katika mchujo wa shindano hilo.

Fainali hizo zilifanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 25,2019 jijini Dar es Salaam ambapo Meshack Fukuta mshiriki kutoka Mbeya aliibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha Sh50 milioni.

Katika fainali hizo kulipambwa na burudani mbalimbali, huku waliowahi kushiriki kwenye shindano hilo wakikutanishwa jukwaani moja.

Waliokutanishwa ni Kala Jeremiah ambaye alikuwa mshiriki wa BSS ya mwaka 2014, Mshindi wa BSS msimu wa kwanza mwaka 2014, Jumanne Iddi.

VIDEO: BSS 2019 yawakutanisha Jumanne Idd,Kayumba, Kala Jeremiah na Angelmary jukwaa moja Mwingine ni AngelMary Kato mshindi wa nne BSS 2015 na Kayumba ambaye ni mshindi  BSS 2015.

Katika usiku huo watatu hawa walipanda jukwaani kwa nyakati tofauti huku kila mmoja akiimba nyimbo zake na pale Kala alipokuwa akimalizia kuimba wimbo wake wa 'Ndoto' ndipo Jumanne, Angel na Kayumba pamoja na washiriki wengine wa BSS kwa mwaka 2018 walipoungana naye kuimba.

Kitendo hicho si tu kiliwafurahisha watazamaji bali na Rita Paulsen ambaye ni muasisi wa mashindano hayo jambo lililomfanya kila wakati kusimama na kushangalia.

Chanzo: mwananchi.co.tz