Mke wa msanii nguli wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay aitwaye Grace Mgonjo ameeleza namna ambavyo wamekuwa wakipokea baadhi ya uzushi wa kifo cha mume wake ambao umetokea mara kadhaa, na kusema kuwa ni jambo ambalo haliwapendezi familia ya msanii huyo.
"Kwa sisi kama mimi na yeye (Mke na Mume) kwetu haitusumbui sana kwasabau ni kitu ambacho kinatokea mara kwa mara,lakini baada ya kuumwa ni ngumu sana kwa watu walio mbali kama dada zake kaka zake wako nje ya nchi wakipata taarifa kama hizo huwa zinawatoa kabisa kwenye mstari.
"Mfano kama dada yake alipata mpaka presha kwaajili ya hizi ishu za kuambiwa kwamba amekufa kwasababu hata ukimwambia kama hajafa huwa haamini anahisi kama tuna mficha, lakini at least mimi na yeye (Prof Jay na Mke wake) ni vitu ambavyo vinatokea tukiwa ndani tunaambiwa amekufa tunashangaa," amesema mke wa Prof. Jay.