Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Uzazi wa mpango kwa panya unakuja

Panya TB Uzazi wa mpango kwa panya unakuja

Wed, 2 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri ya Jiji la New York imetangaza kuanza kuchukua hatua madhubuti kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika Jiji hilo kwa kutumia mbinu mpya ya kuwapa vidonge vya uzazi wa mpango kupitia mitego maalum ya Panya badala ya kuwaua kwa sumu.

Muswada uliopitishwa Alhamisi iliyopita umeidhinisha matumizi ya dawa ya kupanga uzazi iitwayo ContraPest ambayo ndio itayodhibiti panya hao kuzaliana na kuondoa kero ya kuzagaa kwao kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji hilo ambalo sensa ya mwaka 2023 inaonesha lilikuwa na Wakazi zaidi ya milioni nane.

Vidonge hivyo vya ContraPest vitawekwa kwenye mitego maalum ya Panya ambayo itasambazwa katika maeneo yote ya Jiji hilo ambapo inatarajiwa kupunguza uzalishaji wa mbegu za kiume kwa panya wa kiume huku ikiwasababisha panya wa kike kuingia katika hali ya kukoma hedhi.

Panya wa New York ambao Ripoti ya mwaka 2023 ilionesha idadi yao inakaribia milioni tatu katika Jiji hilo, wamezagaa katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye Vituo vya Treni na Mabasi pamoja na kwenye majengo mengine ya makazi na ya biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live