Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwoya alipuka: Sipendi kuambiwa utaona!

UWOYA KITOVU Uwoya alipuka: Sipendi kuambiwa utaona!

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo mwenye jeuri zake za fedha mjini, Irene Uwoya amefunguka kuwa hakuna kitu kinamkera kama mtu kumuambia utaona.

Uwoya amefunguka hayo leo Agosti 2, 2022 kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameposti picha yake moja kali sana kisha akasindikiza na ujumbe huo byuti byuti.

“Hamna kitu sipendi kama mtu anambie utaona …ntaona nin ambacho sijawahi ona MUNGU kaniumba na macho mawili yanaona vzuri sanaaa …wewe Nani? Nakwambia ushindwe kwa jina la YESU…ujumbe umefika na nimekujibu sina jipya la kuona.”

Uwoya hakumtaja ni nani aliyemwambia maneno hayo lakini kwa jinsi inavyoonekana, kuna mtu kamvuruga kwa maneno hayo na kuamua kumchana kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live