Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwoya aingilia kati Sakata la Aristote na Wema

Tangalebs WPanK9Sp8hh3Mrsemr1Ug5Xt Irene Uwoya

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa filamu, Irene Uwoya amevunja ukimya kufuatia sakata linaloendelea mitandaoni linalowahusisha mrembo Wema Sepetu na mfanyabiashara, Aristote ambaye alionekana akiwalinganisha warembo hao.

Katika video hiyo Aristote alisikika akisema kuwa Wema na Irene hawawezi kulinganishwa kwakuwa hali ya Wema kiuchumi kwa sasa si nzuri, hali iliyozua taharuki kwa wengi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Irene ameweka ujumbe unaoonyesha kusikitishwa na kitendo alichokifanya Aristote huku akidai kuwa hausiki kwa namna yoyote na kwamba hakuwahi kumtu amtukane Wema Sepetu

“Nimeona niongee, na nataka niliweke hili wazi na kila mtu aelewe since najikuta nahusishwa kutokana na ukaribu wangu na Aristote, Binafsi Nimesikitishwa sana na maneno yasiyo ya kibinaadamu yaliyotolewa na Aristote dhidi ya Wema, Watu waelewe kitu kimoja leo, Sijawahi kumtuma Aristote amtukane Wema wala mtu yeyote yule, sina ugomvi na Wema na sina sababu ya kufanya upuuzi wa namna hiyo, Nimempigia pia Aristote kuoneshwa kukasirishwa kwangu, na niseme tu hiyo ni MIHEMKO yake yeye, sihusiki na lolote juu ya hayo aliyoyaropoka ambayo yanaleta hata uchonganishi baina yetu kitu ambacho sikifurahii kwakweli, kingine nichukue nafasi hii kukupa Pole Wema kwa haya yaliyotokea, hata mimi ningekuwa wewe ningejiskia kama unavyojiskia, pole sana sana, na zaidi Aristote nathamini upendo wako kwangu lakini ningeheshimu sana kama itabaki sisi na maisha yetu bila kunilinganisha wala kunishindanisha na yeyote yule sababu mimi naishi maisha yangu siko kwenye mashindano na mtu, asanteni wote, One love!!,” ameandila Irene.

Irene na Aristote wamekuwa wakionekana kuwa na ukaribu na hivi karibuni walikuwa wakiweka video na picha mitandaoni zilizowaonyesha wakizunguka maeneo mbalimbali huku wakijivinjari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live