Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwoya, Steven Nyerere waitwa Basata

67054 Uwoyapic

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wasanii wa Bongo movie nchini Tanzania Irene Uwoya na Steve Nyerere wameitwa na Baraza la Sanaa  la Taifa  (Basata).

Wasanii hao wameitwa Basata ikiwa ni siku moja imepita tangu Uwoya kutumia mkutano wa wasanii  na waandishi wa habari kurusha fedha kwa waandishi jambo ambalo limezua mjadala ikiwamo kuonyesha dharau kwa wana taaluma hao.

Katibu wa Basata,  Godfrey Mngereza akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Julai 16, 2019 amesema, “Kweli, tumewataka wafike hapa kesho kwa ajili ya mahojiano, kufuatia kitendo hicho kilichozua mjadala hapa nchini.”

Amesema Uwoya tumemwita kutokana na kitendo chake cha kurusha fedha huku Steve yeye alikuwa kiongozi wa mkutano huo kwa upande wa wasanii.

Katika mkutano huo uliofanyika jana Dar es Salaam Tanzania, wasanii wa Bongo Movie kwa kushirikiana na mtandao wa kuonyesha filamu za Kiswahili ‘Swahiliflix' walikuwa wakizungumzia uzinduzi wa uonyeshwaji wa filamu hizo unatarajiwa kufanyika Julai 31, 2019.

Steve akizungumza na Mwananchi kuhusu kuitwa kwake Basata amesema,“Ni kweli tumeitwa kesho saa 4 asubuhi.”

Pia Soma

Alipoulizwa ameitiwa nini au ni tukio la jana la Uwoya alijibu kuwa, “sifahamu, lakini muhimu kwenda kusikiliza umeitiwa nini.”

Chanzo: mwananchi.co.tz