Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwoya: Simlei mwanangu Krish kimayai

Uwoyaz.png Uwoya na mwanaye Krish

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

IRENE Uwoya ni mmoja wa mastaa wakubwa wa Bongo Movies anayeaminika kuwa na mkwanja mrefuambaye anasema kuwa, pamoja na kwamba ana pesa, lakini kamwe hamlei mtoto wake, Krish kimayaimayai hata siku moja.

Uwoya anasema kuwa, hawezi kufanya hivyo kwa sababu anajua wazi kuna hasara zake. Uwoya anasema kuwa, ana uwezo wa kumnunulia kila kitu cha starehe na anachotaka yeye, lakini ukweli ni kwamba atampa vile vichache na muhimu kwa mtoto basi na si vingine.

“Simlei mwanangu kimayaimayai, Krish nitampa vitu vyote muhimu vinavyotakiwa kwa mtoto asikose kuwa navyo, lakini siyo anavyotaka yeye kwa sababu ameona wenzake wanavyo. Kama simu ndiyo siwezi kumpa mpaka anamaliza shule na kujitambua,” anasema Uwoya ambaye ni mama wa mtoto huyo mmoja aliyezaa na aliyekuwa mcheza soka wa Rwanda, marehemu Hamad Ndikumana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live