Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwoya: OLEMA italeta mapinduzi ya Filamu Bongo

Irene Uwoya Olema Uwoya: OLEMA italeta mapinduzi ya Filamu Bongo

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa kuamkia jana Mwigizaji Staa wa Bongo Movie nchini, Irene Uwoya alizindua filamu yake mpya inayoitwa OLEMA, filamu hiyo imezinduliwa jijini Arusha katika ukumbi wa Regalz Cinema.

Akiidadavua filamu hiyo, Uwoya amesema kwanza ameishuti kwa muda wa miaka miwili na imetumia zaidi ya milioni 180 za Kitanzania.

"Filamu ya OLEMA imetumia milioni 180 na hii ndiyo filamu ambayo inaenda keleta mapinduzi kwenye soko la Filamu kwasababu iko tofauti stori ni ya tofauti sana haijawahi kutokea lakini pia uhusika nilioucheza humo ndani sijawahi kuucheza tangu nimeanza kucheza filamu.

"OLEMA kwa Kimasai ni Kafara, haikuwa rahisi kunyoa kipara lakini nilinyolewa Umasaini kulekule na Wamasai ndio walininyoa kwa kutumia wembe, lakini kwakuwa stori ilikuwa inataka hivyo ilikuwa ni lazima ninyoe," amesema Irene Uwoya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live