Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwoya, Mobetto, Wolper kwenye nyayo za Wema

19937 Uwoya+pic TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Baada ya ndoa yako na Dogo Janja mkatawala mitandaoni. Ilivutia kutazama na kusikiliza suala lenu. Si umaarufu wenu tu, bali tofauti ya umri na mazingira yake kiujumla. Irene Uwoya kwa Dogo Janja? Kwa kipi? Kivipi yaani? Wengi walioumizwa na zali la Dogo kuliko tofauti ya umri.

Hayo maswali wengi wao ulikuwa wivu hasa kwa wanaume wa Dar. Maana kwa mazingira ya Dogo Janja kukamata totoz kama Uwoya si mchezo. Lakini kulimiliki kinikia kama Uwoya siyo kitu rahisi.

Dogo karoga?

Kuanzia urembo mpaka gharama za kuishi na Irene si kwa mwanamuziki anayetegemea shoo za Fiesta. Uwoya ni sawa na makontena yale ya makinikia pale bandarini.

Ndo ukweli kuwa Irene ni staa, mrembo na ana ‘life style’ ambayo mwanaume lazima ujipange kummiliki mazima. Marehemu Ndikumana alijikuta kama kawehuka hivi. Akaishia kutapatapa kwenye viunga vya Kigali mpaka umauti ulipomtenganisha na dunia hii. Uwoya mchezo.

Sasa mtoto wa Ngarenaro na maisha haya vyuma vimekaza eti kajitwisha kinikia lile? Ilibidi watu wapate wasiwasi. Wakaleta maneno kuwa haikuwa harusi ni kamba tu. Mchongo wa mtoko wa ngoma mpya ya Dogo Janja. Mara sijui movie mpya inakuja. Kifupi ni kwamba hakuna ndoa eti. Ndo maana watu walijiuliza ndoa gani hakuna ndugu wala marafiki wa nje ya Tip Top Connection? Irene aolewe Johari asihudhurie? Any way ndo yale ya Ben Pol na Ebitoke. Kiki iliishia kuwa kiki tu lakini malengo hayakutimia kwa sababu ngoma ilibuma.

Mobetto

Okay si kesi. Tufanye Hamisa ni mtoto sana kiasi kwamba alikuwa hajui kama yule ni bwana wa Zari aliyezaa naye. Tufanye Madale alikuwa anajua ile ni hoteli siyo makazi ya mtu.

Au tufanye kwamba ujauzito ule ilikuwa bahati mbaya tu. Au tufanye kwamba huyu ni mwanaume wa kwanza maishani mwake ndiyo maana alipagawa na kapagawa mpaka hii leo.

Wolper

Achana na wanokonoko na wafitini wa uhusiano wa mtu na mtu. Fuata moyo wako mama, maana walisema nendeni mkazaane mjaze dunia. Lakini siyo lazima kuzaliana. Kwani shingapi bana?

Maana hivi sasa uhusiano wa kingono pia ni kwa faida ya kupata pesa, umaarufu na zaidi ni kujipunguzia msongo wa mawazo. Endelea kwa raha zako. Waache wanaosema kwamba unalea ‘viben ten’, wao wamezoea kudanga kwa madanga mazee.

Sasa kwa nini usiutumie wakati uliopo kujipa raha za mwili wako. Yaani wanasubiri uwe ‘umeresti ini pisi’ ili ‘ukashee’ penzi na funza pamoja na sisimizi ardhini? Kwanza umewasaidia sana vijana. Wote wametoka kimaisha kwa sababu ya nyota yako. Yaani wewe una kanyota flani hivi.

Yaani wakiwa na wewe wanaanza kupanda chati ghafla na kupiga pesa, hizo ni baraka kwako ndio maana hutetereki kimaisha. Simamia msimamo huo huo. Hapo kwako ni mtakuja, ataondoka huyu atakuja yule. Maisha kitu gani bwana. Jiachie tu mama.

Wasanii

Wasanii hasa wa Bongo Movie. Mnajitengenezea mauti. Mnajichimbia kaburi ambalo halitafukuliwa hadi kiama. Acheni siasa. Au acheni sanaa. Mkivibeba vyote kwa pamoja hamtakuwa salama. Mtatoweka kabisa.

Msigeuze umaarufu wenu wa sanaa kama kigezo cha kupata madaraka kwenye siasa za nchi hii. Kama hamjatambua bado, mbali ya ugumu wa pesa za hovyo kwa kipindi hiki. Pia siasa za 2015 zilichangia kuwaondoa kwenye ramani. Hata hilo hamjaligundua?

Wasanii mlitengana sababu ya siasa. Mkabaguana na kuwekeana mipaka ambayo mwisho wa siku ni kuua soko lenu wenyewe. Mkajiwekea vinyongo mioyoni mwenu kwa wasanii hawa kuwatenga wale na wale kuwatenga hawa. Kisa siasa.

Katika akili ya kawaida mnashindwa kuelewa kuwa hao wanasiasa wanawatumieni tu kama daraja? Yaani mlipambana kama yatima kutengeneza majina yenu. Mkaheshimika na watu. Mkakubalika na kupata umaarufu mkubwa bila msaada wa wanasiasa. Leo hii badala ya kutulia mle matunda ya mateso yenu ya kuhangaika muda mrefu kutengeneza majina yenu, mnarukaruka kama bisi kusaka machimbo ya siasa.

Ukihama chama kimoja kwenda kingine sawa ila usiongee maneno kuumiza unaowaacha, kuna maisha nje ya siasa.

Hamkatazwi kuwa wanachama wa vyama mbalimbali. Lakini msitumike bila kujielewa na kuishia kupoteza mashabiki wenu. Kama wewe upo CCM kuna mashabiki wako ambao wako Chadema. Walio Chadema kuna wanunuzi wa kazi zenu wapo CCM. Mnapotumika kisiasa mnawabagua mpaka mashabiki wenu. Nchi hii huwezi kufanya biashara ya kuwauzia CCM au Chadema tu. Sanaa ni biashara inayowategemea wafuasi na wanachama wa Chadema, CCM na vyama vyote. Hili zingatieni kwa umakini sana.

Ukijipambanua kama wewe ni wa chama fulani si mbaya. Ila unatumikaje kwenye hicho chama? Kiroho safi ifikie hatua wasanii hangaikeni siku za kampeni tu. Kwa wakati huu kaeni kimya fanyeni sanaa yenu.

Hakuna ujanja. Kama mmeamua kuishi kwa mkate wa siasa basi acheni sanaa. Na kama mnataka kuishi kwa mkate wa sanaa basi acheni siasa. Mkishikilia vyote viwili mtatoweka. Siasa imeteka sanaa ya Tanzania. Hivi sasa wasanii wako ‘bize’ na siasa kuliko sanaa.

Inashangaza kipindi ambacho Rais Magufuli anakemea kuendekeza siasa badala ya kazi, wasanii hawafanyi kazi, wanaendekeza siasa. Badala ya kutafuta unafuu wa maisha kwenye jukwaa la siasa, pambaneni na maisha yenu ya sanaa ili mchomoke kwenye shimo refu la kifo cha sanaa.

Wema

Wema amewaponza wasanii wengi. Kwa sababu umaarufu wake ulichangia kupaisha wanamuziki wengi kimuziki. Wakakariri kuwa huo ndio mtoko. Hizo kiki huja tu hazilazimishwi au kupangwa. Sawa kama ni promo sasa Uwoya kalipwa shilingi ngapi kwa mchongo huo wa kujifanya kaolewa?

Unashangaa Uwoya kuishi kinyumba na Dogo Janja, kwa sababu hujui faida anayopata Uwoya wala Dogo Janja mwenyewe. Kama unataka kujua faida ya Uwoya kuishi na Dogo Janja kaangalie thamani ya Aunty Ezekiel baada ya kujiweka mazima kwa Mose Iyobo. Maisha ya mjini hapa thamani ya Aunty imepanda baada ya kutulia kwa Iyobo, hagusiki kibwege. Ndicho ambacho anakipata hivi sasa Uwoya.

Na hii ni baada ya wote wawili kuona thamani ya Wema alipokuwa anajiweka kwa watu. Anzia kwa Diamond kurudi nyuma achana na hawa kina Idris na mwenzake Calisah. Mwanaume kumtokea demu asiye na mtu ni tofauti na aliye na uhusiano. Kuna thamani tofauti. Mjanja utaelewa.

Janjaro anajua thamani yake baada ya uwepo wa Uwoya kando yake. Tofauti yake inayomfanya awe juu ya Young Killer na Young Dee kimtazamo wa nje ni yeye kummiliki Uwoya. Shoo ya Janjaro bila uwepo wa Uwoya ni nyepesi sana kuliko za sasa akiwa na Uwoya wake ndani ya nyumba.

Ni kama Diamond alipokuwa na Wema. Ulikuwa mwanzo wa kupanda thamani yake kuanzia kwenye shoo mpaka totozi alizomiliki baadaye. Kuna totoz zilimtaka siyo kwa sababu ya muziki wake mzuri, hapana ni kwa sababu alikuwa bwanaake Wema Sepetu. Endelea kuchukulia poa poa tu.

Thamani ya Diamond haikuwa kwenye sauti na midundo tu, uwepo wa Wema ukawa kiini cha yeye kuwa juu ya Belle 9, Barnaba, Rich Mavoko na wenzake. Hili wameliona Janjaro na wenzake. Wanatumia fursa ya kumiliki makinikia kujipandisha kithamani.

Harmonize alipita njia hii kwa kujitwisha Jack Wolper. Hii ilimsaidia zaidi yeye maana Wolper alikuwa juu sana kama ilivyo kwa Janjaro na Uwoya. Wanamuziki wanafaidika lakini pia nje ya boksi kina Uwoya na wenzake wanafaidika sana kuonekana kwao na hawa mabwana wadogo.

Kwa walioshindwa kuelewa Hamisa kuhusudu zaidi kuongelewa yeye na Diamond, sasa wamepata jibu. Huyu siyo Hamisa wa Majizo tena, kapanda madaraja mengi sana. Hakuzaa na Diamond kibwegebwege tu alijua anachofanya. Mungu ampe nini tena?

Wakati unashangaa mastaa hawa kuandikwa kila siku magazetini, kuchambwa mitandaoni lakini hawakomi. Ni kwa sababu hujui wanachopata kwa aina ya maisha hayo. Wanatengeneza zaidi kuliko unavyofikiria, wasipoongolewa wanateseka zaidi.

Anafaidika ‘direct’ kama wimbo wa “Madam Hero” ulivyopanda chati na kupata views YouTube. Bila Hamisa kuwa na muingiliano wowote na Diamond, wimbo na yeye mwenyewe angepuuzwa kabisa. Kuna kufaidika ‘indirect’ hii tuiache kabatini kwanza.

Tofauti ni kwamba Wema alifaidika zaidi ‘indirect’ kwa drama zake za kiuhusiano. Huku wenzake wakifaidika ‘direct na indirect’. Wema hakutaka kutumia mashabiki waliompenda kwa faida akawaacha waishie ku-comments na ku-like picha zake tu mitandaoni.

Chanzo: mwananchi.co.tz