Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwoya Ateketeza Milioni 20 na Wanaume "Wanawake Wanatamani Ufe"

Uwoya 1 1 Uwoya Ateketeza Milioni 20 na Wanaume "Wanawake Wanatamani Ufe"

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UNAAMBIWA Irene Uwoya ametumia zaidi ya milioni 20 kula bata na marafiki zake wanne wa kiume huko Moshi mkoani Kilimanjaro na Arusha.

Imekuwa kawaida ya muigizaji huyo maarufu wa Bongo MovieĀ  kula bata na watoto wa kiume kuliko wa kike, sasa kama ulikua unajiuliza sana kwanini iwe hivyo leo Uwoya katupa jibu hili.

"Watu wanauliza sina marafiki wa kike? Kiukweli asilimia 90 ya marafiki zangu ni wanaume sababu wamenyooka sanaaa ukikosea wanakuchana ukifanya powa wanakupongeza na ukifanikiwa wanakunjua na kufurahia mafanikio yako kama yao, ila wa kike anakuchekea machoni moyoni anatamani ufe... simanishi siwapendi ila napenda tuonane kwa mbali," amesema Uwoya.

Kwa sasa mrembo huyo yupo mjini Moshi ambapo aliambatana na marifiki zake hao kwenye picha hapo kwa ajili ya kufanya party ya kumaliza mwezi Januari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live