Mvivu ni jina flani hivi ambalo sidhani kama mtu atapenda umuite hivyo na akakukubalia kwa sababu ya sifa la jina lenyewe kwamba hapendi kazi, kujishughulisha au kufikiria zaidi juu ya jambo fulani.
Sasa kwa upande wa msanii wa BongoFleva Matonya amefunguka kusema sababu ya yeye kutopenda kuonekana kwa watu ni uvivu, pia amekiri uvivu umemsaidia sana kwenye maisha yake hadi alipofikia kwa hivi sasa.
"Mimi nipo na napatikana, sio kama sitaki mazoea bali maisha ambayo ninayoyaishi ni ya kutulia sio kujificha, nikiwa sina vitu vya umuhimu naona bora nitulie nyumbani mara nyingi pia nakuwa na uvivu japo uvivu wangu unanisaidia, hata biashara zangu hazipaswi kuonekana kwenye macho muda wote" ameeleza Matonya