Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uturuki kuanzisha kituo cha utamaduni Bongo

Uturuki Msds Uturuki kuanzisha kituo cha utamaduni Bongo

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo Oktoba 3, 2023 Jijini Dar es Salaam amefanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu, ambapo wamekubaliana kushirikiana katika eneo la Utamaduni na Michezo.

Dkt. Ndumbaro amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania inaendelea kupiga hatua katika eneo la Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Sekta hizo sasa ni biashara na zinatoa ajira kwa vijana wengi, huku akisema lugha ya Kiswahili inaendelea kukua na kuongeza idadi ya wazungumzaji.

Kwa upande wake Balozi, Mehmet amesema nchi yake inakusudia kuanzisha Kituo Cha Utamaduni hapa nchini, ambapo amesema Kituo hicho kitatoa fursa kwa waturuki kujifunza kiswahili na Watanzania kujifunza Kituruki.

Ameongeza kuwa, nchi hiyo ipo tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya michezo na kwamba Klabu ya Fernabache ya nchini humo ina nia ya kuanzisha academy ya michezo hapa nchini.

Aidha, Mehmet amesema kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo, Timu za Tanzania zitaendelea kupewa kipaumbele kuweka Kambi za maandalizi ya michezo mbalimbali nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live