Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata majibu ya Shilole kuvunjika ndoa yake na Rommy

Rommy X Shiloleee Utata majibu ya Shilole kuvunjika ndoa yake na Rommy

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vipi, wameachana au ni kiki? maswali ni mengi kwa ndoa ya msanii na mfanyabiashara Zuwena Mohamed 'Shilole' na mumewe Rajabu Issa 'Rommy' kutokana na yanayoendelea mitandaoni.

Wawili hao ambao walifunga ndoa Aprili 22, 2021 wameacha maswali kwa mashabiki tangu jana kutokana na yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakidai ni kiki kwani 'Shishi' anataka kuachia wimbo mpya.

Hata hivyo, watu wa karibu wa wawili hao wamesema chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ni wivu wa kimapenzi na Rommy anadai Shilole anachepuka.

Kwenye mitandao ya kijamii kuna video inayomwonyesha Shilole akiwa na mwanaume wamekaa kwa ukaribu huku mezani kukiwa na vinywaji na inadaiwa mwanamume huyo ndiye anayehusishwa anatoka kimapenzi na msanii huyo anayetesa na nyimbo kama 'Kisasa', 'Viuno', 'Mama Ntilie', 'Pindua Meza' na nyingine nyingi.

Mwananchi lilimtafuta msanii huyo ambaye pia anamiliki mgahawa maarufu wa kuuza chakula la vinywaji wa Shishi Food ili kuthibitisha taarifa hizo za kuvunjika kwa ndoa yake na kudai muda wa kuongelea jambo hilo haujafika na atalizungumzia upepo ukitulia.

"Aise sitaki kupokea simu za watu wengi maana nikipokea tu swali linalokuja ni tumeaachana na Rommy. Hivyo, sitaweza kuzungumza kwa sasa, niache kwanza huu upepo upite," amesema Shilole.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live