Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata kifo cha msanii Mohbad Nigeria, sababu 4 kifo chake zatajwa

Mohbad Utata kifo cha msanii Mohbad Nigeria, sababu 4 kifo chake zatajwa

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maandamo makubwa Nigeria katika miji mbalimbali kwa ajili ya kushinikiza haki kwa Mohbad ambaye amefariki Septemba 12, 2023 kwa sababu inayotajwa kuwa ni Msongo Wa Mawazo Na Infection.

Mohbad Alizikwa siku ya pili baada ya kifo chake. Hivyo Jana kulikuwa na maandamo makubwa Nigeria ya kudai haki juu ya kifo cha Mohbad, Watu hawakupendezwa na kitendo cha yeye kuzikwa mapema kabla ya uchunguzi, hivyo mwili wake umepangwa kufukuliwa kaburini kwa jili ya uchunguzi.

Taarifa Zingine Ukiachilia Mbali Sababu Ya Msongo Wa Mawazo Na Infection, Pia Msanii Naira Marley Amehusishwa Na Kifo Cha Msanii Huyo Mohbad.

SABABU YA NAIRA MARLEY KUHUSISHWA NA KIFO CHA MOHBAD

1. Mwaka jana Mohbad alitemana na label ya "Marlians" inayomilikiwa na Naira Marley hii ilifanya wawili hao kutoelewana na kuwa na uhasama mzito. Huku Mohbad alikuwa akidai anapitia wakati mgumu Sana kwa vitisho na hofu anayopewa na aliyekuwa bosi wake ambaye ni Naira Marley.

2. Mohbad aliwahi kuripoti tukio la kuvamiwa location akiwa ana shoot video na watu waliodai kuwa wapo chini ya Naira Marley. Alipewa kipigo cha nusu kufa pamoja na kufanyiwa uharibifu mkubwa Kisha watu hao kuhaidi kumuua.

3. Hivi Karibuni Naira Marley alitangazwa kuwa balozi wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya Nigeria @ndlea_nigeria ambapo muda kidogo shirika hilo liliweza kumkamata msanii Mohbad wakimuhusisha na matumizi ya madawa.

Inadaiwa kuwa baada ya Mohbad kukamatwa alilazimishwa kunywa vidonge ambavyo vinadhaniwa kumletea madhara ya kifo chake. Watu wanadai kuwa huwenda shirika hilo lilitumwa na Naira Marley kumfanyia Mohbad kitendo hicho na hadi sasa ukipita kwenye Instagram yao utakutana na comments kuhusiana na suala hilo.

4. Sababu nyingine ni historia mbaya ya uhalifu aliyonayo Naira Marley pia imepelekea watu kumuhusisha moja kwa moja kwenye kifo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live