Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utanashati wamkosesha dili Mjukuu wa Mwai Kibaki

Andrew Kibaki Utanashati wamkosesha dili Mjukuu wa Mwai Kibaki

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo na mfanyabiashara ambaye pia ni mjukuu wa Hayati Mwai kibaki, Sean Andrew, amefunguka na kuweka wazi kuwa aliwahi kukataliwa kufanya tangazo kisa utanashati (uzuri) aliokuwa nao.

Sean ameyasema hayo katika mahojiano yake na podcast ya Flo & Frens baada ya kuulizwa kuhusu faida na hasara za kazi yake ya mwanamitindo na kueleza kuwa aliwahi kukataliwa katika dili la kufanya tangazo kwa kuwa na muonekano mzuri (handsome).

Ambapo wahusika wa tangazo hilo alilogoma kuwataja walimpigia simu na kumwambia yeye ni mzuri sana hivyo walitaka mtu mkakamavu.

Kwa mujibu wa mwanamitindo huyo alieleza kuwa aliamini kupitia kampuni hiyo ingeweza kumchagua jambo ambalo lilikuwa kinyume. Amedai kuwa tukio hilo lilimkatisha tamaa kwa sababu aliweka matumaini makubwa katika tangazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live