Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Utalipwa Milioni 11 kumshikia mwamvuli rapa Quavo

Tyy556666 660x400 Msanii Quavious Keyate Marshall (Quavo)

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Staa Quavo anaetokea katika kundi la Migos time hii amechukua Vichwa vya Habari mitandaoni baada ya kupost picha kupitia mtandao wa Instagram ikimuonesha akiwa ameshikiwa Mwamvuli na jamaa anaedai kuwa anamlipa Dola 5000 za kimarekani.

Star huyo anamlipa jamaa huyo dola 5000 ambazo ni sawa na Takribani Milioni 12 za kitanzania kwa ajili ya Kumshikia Mwamvuli pamoja na kumpepea ili asihisi Joto.

Quavo amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika kuwa Anamlipa msaidizi wake huyo Pesa hizo kwa Siku moja.

Jina halisi la msanii huyo ni Quavious Keyate Marshall ni mzaliwa wa Marekani mnamo April 2,1991. Msanii huyo ni muimbaji, mwandishi wa nyimbo na Mtayarishaji wa muziki.

Chanzo: millardayo.com